Christian Bella – Pacha Lyrics

Christian Bella Pacha Lyrics

Christian Bella – Pacha Lyrics

Christian Bella Pacha Lyrics

Kila ukweli sio lazima useme
Ikizidi sana lazima ufunguke
Nilikuwa dhahabu mikononi mwa kipofu
Hakujua dhamani yangu alinidharau

Udongo wa mfinyanzi aridhini
Kujua dhamani yake waulize wafinyanzi
Nishapata pacha wangu wa milele
Katambua dhamani yangu tunapendana

Pacha ni moja ya madini
Mola baba alificha mbinguni
Umeshushwa chini ili uwe wangu tu
Sauti tamu kama nyoya linachokonoa sikio
Mikono yako inanimaliza homa bila dawa
Ndo maana nakupendaga sana

Mi nakupenda baby aah baby
Nimepata pacha ujue
Mi nakupenda baby aah baby
Aah pacha pacha wee

Mi nakupenda baby aah baby
Raul mashubedi modern fashion

Nani mwenye kipimo cha mapenzi alete
Nipime watu wote waone
Yes mimi, ju mapenzi ananipaga mimi
Mimi mimi …

Pacha pacha wangu we
Mshumaa bei rahisi
Unaweza unguza nyumba ya mabilioni
Chungana na maneno ya wapambe

Yanaweza haribu penzi letu
Mtoto wa mama eeh
Si unajua fresh (Fresh fresh fresh)
Nakupendaga sana, mwana mama eeeh

Bado pacha usisahau

Mi nakupenda baby aah baby
Nimepata pacha ujue
Mi nakupenda baby aah baby
Aah pacha pacha wee

Mi nakupenda baby aah baby
Bill Gate Katunzi, mzamili

Nani mwenye kipimo cha mapenzi alete
Nipime watu wote waone
Yes mimi, ju mapenzi ananipaga mimi
Mimi mimi

Written by; Christian Bella
Released date; 23 September, 2020

    Lyrics Details:

  • Written by:
  • Album: